“Tunasafiri pamoja, katika chombo cha anga, huku tukitegemea hifadhi ya hewa na
udongo; sote tunahakikisha usalama wetu kwa kudhibitisha amani na mahala pasipo na
hofu; kulindwa dhidi ya uangamizi kwa kuendeleza utunzaji, bidii kazini na,
nitasema, upendo tunayoipa ufundi wetu dhaifu. Hatuwezi dumisha chombo hiki kwa
mbinu zilizo nusu bahati, nusu huzuni, nusu ujasiri, nusu kukata tamaa, nusu utumwa
wa maadui wa kale wa binadamu, nusu huru katika ukombozi wa rasilimali zilizokuwa
ndotoni pekee hadi siku hiyo. Hamna ufundi wala wafanyi kazi walioweza kusafiri kwa
usalama katika utata mkubwa wa kiwango hicho. Kuishi kwetu wote unategemea utatuzi
wao.” - Adlai Stevenson.
Katika safari yetu, binadamu amekosa kutii mashauri haya na sasa yumo katika njia
panda iliyohitaji tuweze kubadilisha mwelekeo kwa haraka ndipo tuweze kujiokoa kabla
wakati udidimie.
( 1a)(4,5).
Wakiwa katika mji wa Kairo, mwaka wa 1994, Umoja wa Mataifa ulikubali kwa kauli moja
kwamba idadi kubwa sana ya watu ndio tisho kubwa zaidi ambayo watu wamekabiliana
nayo (1). Mataifa mengi hawakutii
maazimio ya Umoja wa Mataifa na hivyo vitisho vya binadamu na mazingira vimeongezeka
na kuhitimu viwango ambavyo uwezo wa dunia kuendeleza maisha umepita mipaka
(2)(29a)
Tunarufaa kwenu kama wanachama wa kizazi cha sasa wa mwananchi husika kwa sababu
tunaamini ya kwamba unajali. Suluhisho la haraka ni kukuza elimu kuhusu: familia,
mipango, afya, ubaguzi wa rangi, uchumi, nishati mbadala, kuhamasisha na kuwezesha
wanawake na uhifadhi wa mandhari (2a)
Hii itasababisha athari kubwa chanya kwa binadamu na kwa mandhari ambayo maisha
yote inategemea. Tishio kubwa kwa kuwepo wetu si ugaidi, vita, au madawa ya kulevya.
Tishio kubwa ni kupungua kwa maliasili na uchafuzi iliyotokana na kuongezeka kwa
mahitaji ya binadamu
(3).
Idadi kubwa ya watu ndiyo chanzo cha ukosefu wa ajira, njaa, uhalifu, madawa ya
kulevya, ushirikiano wa familia, ugaidi na vita. Wataalam wanatabiri ya kuwa
tukiendelea kuongezeka, binadamu hataweza kuishi duniani kwa miaka mia moja
tusipoungana na kutatua hii shida kwa haraka
(3a,3b).
Hapo zamani, katika miji na mashamba kote nchini, kazi ya mikono ilikuwa tele,
iliyohitaji familia kupata watoto wengi ili waweze kusaidia kufanya kazi. Wanaume
waliitunza familia, na wanawake walibaki nyumbani kulea watoto, kuhudumia wazee na
wagonjwa. Waliweza kupata nafasi ya kukaa na familia yao, pahali ambapo mahitaji ya
kihisia yalitimizwa. Wakati huo upendo na heshima ilikuwa kawaida, matatizo ya
kisaikolojia na madawa ya kulevya yalikuwa nadra. Watu waliohitaji usaidizi waliweza
kutegemea usaidizi kutoka majirani kwa sababu hisia ya huruma na jamii
ilitawala..
Katika ujio wa mapinduzi wa viwanda, watu wengi walipoteza kazi baada ya uvumbuzi wa
mashini, na hivyo mashindano ya ajira ilikuwa jambo la kawaida. Bidhaa zilizoweza
kununuliwa na matajiri pekee wakati uliopita, ziliweza kununuliwa na watu wengi
nchini kwa sababu mitambo na maliasili nyingi ilileta bei ya bidhaa chini. Biashara
zilihimiza, “NUNUA. NUNUA, NUNUA!” kwa watu wote, na kuwezesha wakati wa ulaji na
mashindano kati ya watu. Huu mtindo wa maisha ulihamasisha wanawake kujiunga na
waliofanya kazi ili kupata riziki. Ulimwengu wetu mpya umekuwa wa mashindano na
kukosa upendo, mahala ambapo wanaofaulu huishi vyema na, kwa upande mwingine,
uhisani na uungwana umepungua. Kwa mfano, katika mitaa mingi, ni haramu kuwapa
maskini na watu wasio na makazi vyakula na malazi (6 ,7 ).
Haya ni Dalili za Idadi Kubwa ya Watu
Dalili za idadi kubwa sana ya watu nchini zinafaa kufahamiwa ndipo tatizo hili
lisuluhishwe. Leo, katika familia, waume na wake wanafika nyumbani baada ya kazi huku
wamechoka kihisia na kimwili, na ndivyo huzua hoja kati yao mara nyingi; hawapati wakati
wa kuwa kivyao wala wakati kuwa na familia yao. Watu wachache wanafunga ndoa sasa, na
kiwango cha talaka kimeongezeka kwa miaka 50 iliyopita. Kwa mfano, nchi ya Belarus
iliripoti kiwango cha talaka 50% mwaka wa 2012 (
8). Mauaji ya watoto wachanga ndiyo sababu
ya kwanza ya vifo vya kikatili ya watoto nchini Amerika (
9,
10). India ina visa vinavyoashiria kuongezeka
kwa kiwango cha kujiua kwa sababu ya ukosefu wa njia za kuweza kujikimu na ajira (
11).
Shinikisho linalotokana na ukosefu wa ajira linasababisha watu wengi kugeukia madawa
dawa ya kulevya na pombe kama misaada. Kinyume cha hayo, Japani, nchi iliyokuwa
mojawapo kati ya nchi yenye viwango vya juu zaidi vya kujiua, inaonyesha ongezeko la
kiwango cha ajira tangu 2011 kutokana na kupungua kwa idadi ya watu. Kiwango cha
kujiua kimeshuka, na hivyo mashindano ya ajira imepungua (12). Uchina, pamoja na sera yake ya
mtoto mmoja kwa familia, ilitoka katika taifa ambalo njaa iliangamiza mamilioni ya
watu, na kuwa taifa la pili tajiri zaidi duniani (13). Walakini, sera ya Uchina ya
mtoto mmoja iliunda kizazi cha watu wenye ubinafsi, wanaopenda mali ambao hawana
hisia ya jumuiya ambayo familia ya watoto wawili hutoa (14).
Usawa sahihi kati ya maliasili na ukubwa wa idadi ya watu yafaa kuwa ili tuweze
kukuza ustawi, fursa za elimu na ajira. Kazi ndiyo chanzo cha kile ambacho kinawapa
binadamu maana yao ya kusudi, hadhi na thamani. Hivi vitu ndivyo msingi wa kiuchumi
na utulivu wa kijamii. Uchumi duni, kwa upande mwingine, inawezesha ugaidi, ubaguzi
wa rangi na uasi inayosababisha mauaji ya kimbari au vita.(14a,14b)
Katika dunia hii ya matumizi ya bidhaa, watu hawana wakati wa kuwa na wengine, kwa
hivyo ni rahisi kuwapa watu vitu vya nyenzo kuliko kuwa nao. Mwishowe, watu wa
kizazi kipya wanathamini mafanikio na tuzo kwa suala la nyenzo. Si jambo la
kushangaza ya kwamba uyakinifu unachukua nafasi ya mguso wa kibinadamu, ilhali
hautimizi mahitaji ya kihisia. Watoto na wanandoa wanaohitaji upendo wa kibinadamu
na wanaoikosa manyumbani wanaitafuta mahali pengine. Inaelezea sababu ya mimba za
utotoni kufika milioni 16 ya watu wanaozaliwa kila mwaka ulimwengu mzima (15). Huko Marekani, 40% ya akina mama
wapya hawajaolewa(16). Wakati huu, jamii yetu yenye msongo
wa mawazo, inachora picha ya ngono kuwa mtindo mwema.
Ngono imekuwa jambo lenye wengi waliloizoea wanatafuta mapenzi na mahaba ndipo
waweze kutoa msongo wa mawazo. Jambo hili lilikuwa dhahiri zaidi baada ya Vita vya
Pili vya Dunia, iliyosababisha kuzaliwa kwa watoto wengi. Dhana ya kuwa vita
husaidia kwa kudhibitisha kuwa ukubwa wa idadi ya watu iko sawa, ni makosa. Katika
mwaka wa 1800, idadi ya watu duniani ilikuwa bilioni 1.3 na idadi ya watu huko
Marekani ilikuwa milioni 5. Mwaka wa 2023, idadi ya watu duniani ni bilioni, 8.045
na idadi ya watu Marekani ni milioni 336, 704 (17).
VVita, majanga, magonjwa, na vifo vya asili, kwa upande mwingine, haijaweza kupungua
ongezeko la watu. Katika mataifa maskini, familia nyingi wana watoto wengi kuliko
wanavyoweza kuwakimu na kuhakikisha ya kwamba wanaishi (18). Duniani, watu wa kiasili karibu
milioni 370 na watu maskini bilioni 2.6 wanaishi bila stima, maji na vifaa na
kadhalika (Ona jalada la Lifewatchgroup.org’s web site - NASA NIGHT LITES) (19,20)na watu mamia ya mamilioni
hawawezi kupata vyanzo salama vya maji ya kunywa (21). Watu hawa wangepata nafasi ya
kuishi maisha ya kisasa kama watu walioishi kwa mataifa yaliyoendelea, ingechukua
sayari tano 5 kututegemeza sisi sote (22). Kunao
makabila ya watu ambao hawana mawasiliano na ulimwengu wa kisasa, ambao wana furaha
na wanastawi. Hawapati matatizo ambazo ulimwengu wa sasa wanakabili. Wanafurahia
maisha kwa sababu wana hisia ya jamii na heshima kwa raslimali. Hii inathibitisha ya
kwamba pesa, kuishi kwa ulimwengu wa kisasa na uyakinifu sio jibu (22a).
Ustaarabu ilibadilishwa Milele na Vita vya Pili vya Dunia, Mapinduzi ya Viwanda na
Kisayansi
(Angalia grafu hapo juu)
Mapinduzi ya viwanda na ya kiteknolojia yanazidi kuchukua nafasi ya binadamu kupitia
vyombo, tarakilishi na roboti. Watu wamelazimishwa kukosa ajira kabisa kwa namna
haijawahi kuwa kwa wakati wowote uliopita na inasababisha pengo kubwa kati ya
matajiri na maskini. Sheria zinazohimizi upendeleo kwa wanaadamu kuliko vifaa lazima
zitekelezwe; tusipofanya hivyo hali hii itasababisha njaa, kuleta hasara, upinzani,
ukatili wa polisi, ubaguzi wa rangi na ugaidi.
Historia inatufunza ya kwamba makundi ya watu wenye njaa waliangamiza miliki ya
Warumi, Wafaransa na Warusi. Wakati wa sasa, bomu la wakati iliyosababishwa na
kuzidi ya idadi ya watu ni uhaba wa chakula na ukosefu wa ajira, itakayowezesha
matukio sawa na hayo kufanyika (23).Umaskini na kupungua kwa
maliasili inasababisha watu kujidhalilisha wenyewe na kutoweza kujikimu. Kutokana na
uharibifu wa mazingira, makundi ya watu wanahama kutoka nchi yao na kwenda kwa
mataifa jirani, pahali ambapo wana matumaini ya kwamba watapata riziki. Hii
ilisababisha ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya wageni kwa wakimbizi wa taifa
kutafuta makazi kutokana na hofu ya uharibifu wa ustaarabu katika hilo taifa. Huku
uhalifu ukiongezeka, mataifa hugeukia vita wakitafuta bidhaa. Ripoti ya mwaka 2015
inaashiria ya kwamba zaida ya theluji moja (1/3) ya watoto duniani wanakufa kila
mwaka kutokana na utapia mlo (24).
Marekani, moja kati ya watoto sita hulala njaa kila usiku (25,26). Mpango wa
Chakula Duniani unabainisha ya kuwa: “Inatarajiwa kuwa watu milioni 345.2
watakuwa
na uhaba wa chakula mwaka wa 2023 – mara mbili zaidi ya nambari iliyotarajiwa
mwaka
wa 2020. Hii inahususishwa na ongezeko kubwa ya watu milioni 200 ikilinganishwa
na
viwango kabla ya COVID-19. Zaidi ya watu 90,000 duniani wanapambana kuishi
wakati wa
njaa. Hii ni mara kumi zaidi kuliko ilivyokuwa miaka mitano iliyopita.”
(26a)
Ili waweza kupata ajira, wakulima wanalima ardhi na wanafuga mifugo kwa shamba yao
kupita kiasi. Hii inasababisha mmomonyoko wa udongo na kuenea kwa jangwa. Ardhi
nyingine inachukuliwa ili itumiwe kwa makazi, uchimbaji madini, ukataji miti,
ukulima, mibwawa ya maji (kwa hifadhi ya samaki), jambo ambalo linaangamiza aina za
wanyama pori na mimea (27) na kulazimisha
uhamiaji wa watu wengi
(28).
Wataalam walithibitisha ya kwamba dunia inaweza kukimu karibu watu bilioni 6.2.
Tumepitisha hii nambari, kama ambavyo kufa kwa binadamu 2% kwa miaka 15 iliyopita
inathibitisha (29,29a).
Licha
ya hayo,
idadi ya watu inaendelea kuwa kubwa. Tusipotatua mashida haya, hali itazidi kuwa
ngumu na wakati unadidimia.
Ripoti za Umoja wa Mataifa zinaashiria ya kuwa tangu miaka ya 1990, karibu 50% ya
wale walioishi kwa chini ya USD $1 kwa siku wanaishi kwa kiwango juu ya hii kiasi
cha pesa sasa, kwa hisani ya juhudi za kuelekeza mgawanyo sawa wa mali na elimu,
juhudi hizi zilizokuzwa na Umoja wa Mataifa, serikali nyingi na Mashirika Yasiyo ya
Kiserikali. Kutokana na ongezeko kubwa la watu, nambari asili ya watu maskini
haijapungua. Benki ya Dunia inaelezea jambo hili: “Ingawa kiwango cha ukuaji wa
idadi ya watu ya nchi zinazoendelea imekuwa ikipungua kwa miongo kadhaa, idadi ya
watu imeongezeka zaidi ya wale waliomo kila mwaka. Idadi hii kuongezeka
imesababishwa na idadi msingi ya watu kuwa kubwa.”
(30).Ongezeko hili
imeonekana katika tabaka la kati, inasababisha ulaji, na hivyo kuzidisha uharibifu
wa mazingira, na kukosa kuwezesha wakati wa maandhari kujaza na kustawii (31). Hii utajiri mpya inaonekana kwa
ladha inayoongezeka ya matumizi ya vyakula visivyo sindika na ya wanyama. Kukidhi
mahitaji ya bidhaa ya wanyama, ufugaji unatumia 40% ya ardhi duniani na 60% ya
nafaka za kulisha mifugo (kuku, samaki, wanakondoo, mbuzi n.k.); biashara ya kilimo,
inatumia 70% ya maji safi yanayopatikana (32) .
Watu maskini wanatengwa kwa biashara ya kilimo kwa sababu ni faida zaidi kulisha
mifugo kuliko kulisha watu maskini. Maendeleo ya kisayansi inayoangazia uzalishaji
wa chakula, biashara ya kilimo imekua na kwa sasa imesababisha 50% ya ongezeko la
joto duniani (33).
Chakula Kizima, Lishe Inayotegemea Mimea Hulinda
Afya ya Binadamu Mali na
Mazingira ( 33a ,33b )
Kulingana na Shirika la Afya Ulimwenguni, lishe inayotegemea wanyama ya: nyama ya
wanyama, samaki na vyakula vingine vya baharini, mayai na maziwa inasababisha 63% ya
maafa katika dunia iliyoendelea (34). 90% ya hizi kesi: ugonjwa wa
moyo, kiharusi na saratani, aina ya pili ya ugonjwa wa bolisukari, ugonjwa
autoimmune na Ugonjwa wa Alzheimer zinahusishwa moja kwa moja na bidhaa ya wanyama
na vyakula vya kusindika (34g)
Mageuzi ya binadamu inaashiria ya kwamba binadamu kwa njia kubwa ni walaji wa mimea (34a, 34a1) na biokemia ya
binadamu bado haijabadilika kwa namna ya kuweza kukabiliana na lishe ya wanyama,
jambo ambalo linaloeleza viwango vya juu ya magonjwa na vifo vya binadamu
(34b, 34c). Ushahidi wa
kupungua mwendo wa mabadiliko ya mageuzi ni kwa mfano, wakati ambapo wagonjwa
wanapopata magonjwa yaliyosababishwa na vyakula kama ugonjwa wa moyo, na wakose kula
vyakula vyenye lishe ya wanyama (kama maziwa, samaki, mayai) na chakula cha
kusindika, wanarudi sawa na wanapona (34d, 34e, 34f).Magonjwa haya yanayohusiana na
vyakula au lishe yanasababisha athari kubwa kwa gharama ya huduma ya afya na tija.
Kwa mfano, katika mwaka wa 2014, gharama za kibinafsi na za serikali kwa huduma za
afya Marekani zilikuwa mara tano zaidi ya gharama zake za kijeshi
(35,35a,35b, 35c). Suluhisho
ni rahisi: badilisha menyu iwe nafaka zisizochakatwa, matunda, kunde, mizizi, na
mboga. Wakifanya hivyo, athari ya uponyaji kwa afya ya mtu itathibitishwa kwa muda
isiyokuwa chini ya miaka miwili
(36,37,37A)
Pata SUBTITLES chini ya video bonyeza CC, kisha bonyeza, , hapo bofya SUBTITLES
,
kisha, ⚙ tembeza na ubofye Kiswahili
Kumbukumbu ya filamu, “GAME CHANGERS’ inathibitisha kuwa walio na afya na nguvu zaidi
ndio wenye hula mimea nzima, lishe wa aina isiochakatwa. Kuboresha afya yao, Arnold
Schwarzenegger, mshindi wa cheo, Mr. Universe n.k. na gavana wa mji wa California,
na Rais Bill Clinton walifuata mtindo huu mpya yenye afya.
Ongezeko ya Idadi ya Watu, Lishe Isiyofaa na Ulaji
Huleta Madhara
Idadi ya watu inayoongezeka inazidisha uchafuzi, kutia kemikali iliyo na sumu
shambani, anga, na maji, huku ikiangamiza kiini cha maisha. Hii inasababisha
ongezeko la joto duniani, jambo ambalo linazidisha mafuriko, ukame, maporomoko ya
matope, moto wa misitu na dhoruba n.k. Matukio haya yanasababisha jangwa, uyeyushaji
wa barafu, kupanda kwa viwango vya bahari, na kuteketeza usambazaji wa maji safi,
kwa kasi na kwa kiasi ambacho husababisha matokeo yasiyoweza kurekebishwa
tusipochukua hatua ya kuyakomesha sasa.
TTuna ujuzi na fedha. Suluhisho hili linahitaji ushirikiano duniani, la sivyo, juhudi
ya watu wachache hazitafaulu. Ni muhimu tuwezeshe wanawake wapate elimu, ujuzi wa
kupanga uzazi na kupata namna tofauti wa kupanga uzazi, kufuata kanuni za maadili na
za kibinafsi za kidini, ili wasihitaji kutafuta njia za kutoa mimba, kwa sababu
kuzuia ni bora kuliko mambo yote (37a)Kupiga marufuku kwa njia halali
ya kutoa mimba inaongeza viwango vya vifo vya uzazi, jambo linalotenga yatima na
kuwawacha nyuma (37b)
Kwa kila $1, serikali inatumia kwa njia za kuzuia mimba, $7 inahifadhiwa(38) Tunafaa kupa ruzuku njia za kupanga
uzazi kutumia mfano wa Thailand. Bado tuna uwezo wa kufikia mustakabali endelevu
tukihakikisha ya kwamba kila familia mpya waelemishwe kuhusu jambo hili muhimu
(38a). Huko Thailand, kutumia elimu na
ruzuku, njia ya kupanga uzazi ilikubaliwa na kutekelezwa. Hii ilibadilisha uchumi,
mazingira, na elimu yao sana mpaka kwa muda wa miaka tano, Bloomberg ilikabidhi
Thailand cheo cha “Nchi Yenye Furaha Zaidi Duniani”(38b).
Tazama namna Thailand, bila kulazimishwa, ilitimiza hili lengo: (38c)
Pata SUBTITLES chini ya video bonyeza CC, kisha bonyeza, , hapo bofya SUBTITLES ,
kisha, ⚙ tembeza na ubofye Kiswahili
Ulaji na kanuni za benki zisizokuwa na sera za maendeleo zimezorotesha maisha ya watu
kifedha, mashirika na mataifa (Nchi za Ugiriki na Iceland ni mifano hapa) (39).Mapato ya usawa, kodi za ongezeko
la thamani, kanuni za haki za benki na kuzuia mashirika kupata hadhi kama watu,
inahitajika ili waweze kukomesha kuporomoka kwa uchumi, kuwezesha athari chanya
katika usambazaji wa mali na njia ya matumizi ya fedha (40, 41).Tunafaa
kukomesha ruzuku ya vyanzo vya sumu vya chakula, vyanzo vya sumu vya nishati. Sisi,
kama Thailand, tunafaa kuweka ruzuku kwa njia za mpango wa uzazi. Tunafaa kuhimiza
nguvu mbadala iliyo safi. Lazima tujifunze kuwa wasimamizi wazuri wa ardhi, ambayo
itahitaji kutathmini bidhaa kwa kuzingatia gharama halisi ya kuzalisha na kuzitoa
kutoka kwa mazingira yetu kulingana na athari za uharibifu wa mazingira na matatizo
ya afya ambayo yanahusisha. Zaidi ya yote, tunapaswa kujifunza kuishi kwa
kihafidhina. Utekelezaji wa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) utakatisha tamaa ya
kuchafuka na kuchafua, kuzuia maisha yasiyo endelevu.
Hitimisho
Sasa tunajua ya kuwa hatuna wakati wa kupoteza. Tunajua kile tunachopaswa kufanya na
kufanya hivyo kwa haraka.
Ukuaji wa idadi ya watu inaharibu maliasili, inabadilisha mifumo ya hali ya hewa, na
inasababisha kutoweka kwa wingi wa mimea na wanyama, jambo ambalo si endelevu kwa
wote. Kwa kufanya hivyo, hii inahatarisha uhai wa binadamu na uhai wote kwenye dunia
yetu dhaifu. Njaa inayotokana na uharibifu wa mandhari inasababisha kuongezeka kwa
utumizi wa madawa ya kulevya, uhalifu, ukosefu wa makazi, kupigana wa kijamii, chuki
dhidi ya binadamu, na ubaguzi wa rangi inayokomesha maelewano na amani. Pamoja na
elimu na upangaji wa uzazi, riziki na urejesho wa mazingira yaliyopotea inaweza
kutimizwa (42) Kubadilisha
lishe yetu ya mimea mzima, vyakula ambavyo havijasindikwa vitaboresha afya yetu na
kutupa fedha ili tuhitimu: huduma ya afya kwa wote, elimu, kurejesha mfumo wa
ikolojia, utafiti kwa ajili ya kurekebisha na kuunda teknolojia ya ufanisi
itakayomaliza uharibifu wa mazingira. Tukizingatia haya, tutapata wakati wa
kuhakikisha kwamba binadamu watafuata njia ya uendelevu na amani.
Kwa kuwezesha watu wetu wapate kazi badala ya kutumia vifaa, tutaweza kuboresha hali
yenye binadamu huishi na kurejesha utu wa binadamu. Kwa kubadilisha dhana, tutapata
nafasi ya kurejesha hisia za jumuiya na maelewano. Kwa kuhamasisha amani, fedha za
kijeshi zitatolewa kwa ajili ya maendeleo ya wote (43,44).
Tunapoangazia ulimwengu usio na mwisho, tunajua ya kuwa dunia ndio pahali pekee
panapoweza kutukimu. Bahari za matatizo imepeleka chombo chetu dhaifu mahala ambapo
tumeelewa ya kuwa tukiwa pamoja, ndivyo tutaweza kuokoa hazina kuu kuliko yote –
maisha yenyewe. Tunajifunza ya kuwa tukiwa pamoja kama familia duniani, tutaweza
kuwapisha kizazi kipya tochi ya maisha. Njia hii itahitaji kuacha nyuma ubinafsi,
siasa na tamaa. Tukibadili mienendo yetu na kuheshimu yote yaliyoumbwa na Mungu,
kizazi kipya itarithi dunia ambayo nyimbo ya ndege za mwituni na marashi
yaliyotokana na maua ya msitu inatupa furaha kwa mioyo yao, mahali ambapo watapaita
NYUMBANI(45) mahali
ambapo wote wanaweza ishi kwa heshima na amani.
*Benki kuu ya Dunia
inaeleza umaskini wa wastani kuwa: kuishi kwa $1 - $2 kwa siku
**Ufafanuzi wa Tume ya
Dunia ya Mazingira inaeleza neno endelevu kuwa: Jamii endelevu ni jamii mojawapo iliyo
“timiza mahitaji ya sasa bila kuafikiana na uwezo wa kizazi ijayo kutimiza mahitaji yao
wenyewe.